News

TANGAZO LA MAHAFALI

Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wanafunzi wote waliomaliza masomo yao katika mwaka wa masomo wa 2017/2018 kuwa Mahafali ya KUMI na maadhimisho ya miaka kumi(10) ya Chuo kuwa Wakala wa Serikali yatafanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa tarehe 20 na 21 Desemba 2018 katika Kampasi ya Ubungo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo atakuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Prof. Makame Mbarawa. Aidha wahitimu wanaotaka kushiriki Mahafali hayo wathibishe ushiriki wao kwa Msajili wa Wanafunzi kupitia registrar@waterinstitute.ac.tz kabla ya tarehe 18 Desemba 2018.

Mazoezi ya mahafali hayo yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 Desemba, 2018 saa nane na nusu mchana Chuoni.

Nyote mnakaribishwa.

IMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA CHUO

Posted on 06th December, 2018