MABADILIKO YA RATIBA YA KUFANYA MITIHANI YA SUPPLEMENTARY NA SPECIAL KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, anawataarifu Wanafunzi na Walimu wote wa Chuo cha Maji kuwa, kutokana na tukio la kitaifa la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23/8/2022, tumefanya mabadiliko ya ratiba ya kufanya mitihani ya supplementary na special.Mitihani hiyo iliyokuwa inafahamika hapo awali kwenye kalenda ya Chuo kuwa itaanza tarehe 22/8/2022 hadi 26/8/2022, baada ya kufanya mabadiliko, sasa itaanza tarehe 15/8/2022 hadi 19/8/2022.
Walengwa wote mnatakiwa kuyatekeleza maelekezo haya kwani hakutakuwa na nafasi nyingine ya kufanya mitihani hiyo nje ya tarehe tajwa hapo juu.
Tunawatakia utekelezaji mwema wa maelekezo hayo.