Mahafali ya 46 ya Chuo cha Maji

Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wahitimu, wanafunzi, watumishi, wadau na watu wote kuwa sherehe za Mahafali ya 46 ya Chuo cha Maji yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 24/11/2022 kuanzia saa 3:00 Asubuhi katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia tangazo hili, wahitimu wote mnatakiwa kupitia orodha ya majina yenu iliyopo chini kwenye tangazo hili na kuhakiki majina hayo yafanane kama yanavyosomeka katika cheti cha kidato cha nne. Marekebisho yote yatumwe kwa barua pepe kwenda registrar@waterinstitute.ac.tz.

Aidha, wahitimu mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu kupitia account zenu za SIMS na kufanya malipo ya Tshs 35,000/= kabla ya tarehe 10/11/2022. Kwa atakayehitaji kutumia fedha za tahadhari ambazo ni Tshs. 30,000/= atahitajika kilipa Tshs. 5000/= tu kufanya uthibitisho huo.

wote mnakaribishwa.

Bonyeza link kupakua majina ya wahitimu