News

Hafla ya makabidhiano ya Kituo cha Utafiti cha Ngurudoto kwa Chuo cha Maji

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb) ametimiza ahadi yake aliyoitoa ya kukikabidhi kituo cha Utafiti cha Ngurdoto kwa Chuo cha Maji tarehe 27/02/2022
Hafla hiyo imefanyika Mjini Arusha katika viwanja vya kituo hicho na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Aidha Mhe Waziri amemtaka Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia kuhakikisha analeta ubunifu mpya wa kusaidia changamoto za sekta ya maji zinapata ufumbuzi na kuleta tija kwani kituo hiko kimefika mikono ya watafiti mahiri wa Chuo cha Maji. Mwisho amepongeza mabadiliko ya Chuo kwani sasa kinaendelea vizuri na majukumu yake.

Posted on 28th February, 2022