News

HATIMAYE MALI YA ENEO LA CHUO CHA MAJI NDANI YA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU VYARUDI RASMI KATIKA MILIKI YA CHUO

Baada ya mgogoro wa muda mrefu uliokuwepo baina ya Chuo na Tanesco juu ya umiliki wa eneo na nyumba za Chuo ndani eneo la Bwawa la nyumba ya Mungu Wilayani Mwanga, jana tarehe 25/01/2021 Taasisi hizo ziliingia katika historia mpya ya kumaliza mzozo huo kwa makubaliano ya kuwekeana mipaka halali kwa kila upande. Makubaliano hayo yalishuhudiwa na kuongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Ndg. Zefrin Lubuva.Taarifa kamili ya jambo hili la kihistoria itakujia punde na mkakati wa Wizara na Chuo juu ya matumizi ya kampasi hii katika kutoa mafunzo kwenye sekta ya maji. Tunaendelea kutekeleza maagizo ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (MB) ya kurejesha mali zote za Chuo cha Maji katika miliki yake

Posted on 26th January, 2021