News

Makubaliano ya uendeshaji Kampasi ya Singida

Kazi inaendelea!
Historia imeandikwa jana tarehe 13/04/2021 ambapo Chuo cha Maji na Bodi ya Maji Bonde la Kati wamesaini mkataba wa makubaliano ya pamoja katika kuendesha Chuo cha Maji Kampasi ya Singida kilichopo ndani ya ofisi za Bodi hiyo. Kampasi hiyo itaanza kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Stashahada baadae mwaka huu 2021.
Kwa kipekee Chuo cha Maji tunatoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Bonde la Kati Mhandisi William Mabula na timu yote kwa ujumla, kwa mchango wa kipekee katika kuhakikisha kuwa Chuo kinaanza kutoa mafunzo hayo mwaka huu.

Posted on 14th April, 2021