CHUO CHA MAJI CHAFUNGUA TAWI SINGIDA NA MWANZA
Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wadau wote wa Chuo na wananchi kwa ujumla kuwa Tarehe 22/4/2020 Chuo cha Maji kimefungua rasmi Tawi lake mkoani Singida.
Tawi
lipo ndani ya ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati pembeni ya Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira-Singida mjini.
Huduma
zinazotolewa kwa sasa ni kozi za muda mfupi na huduma ya Ushauri wa Kitaalam
katika sekta ya Maji.
Chuo
kinawahakikishia ubora wa huduma za mafunzo za hali ya juu kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Singida, Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la
kati pamoja na wadau wengine wa sekta ya maji. wadau na wananchi wote,
Pia,
Mkuu wa Chuo cha Maji anayofuraha kuwatangazia kuwa kuanzia Tarehe 24/4/2020
Chuo cha Maji kimefungua rasmi Tawi lake mkoani Mwanza.
Tawi
lipo ndani ya ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Igogo-Mwanza.
Huduma
zinazotolewa kwa sasa ni kozi za muda mfupi na huduma ya Ushauri wa Kitaalam
katika sekta ya Maji.
Chuo
kinawahakikishia ubora wa huduma za mafunzo za kwa kushirikiana na Ofisi ya Bodi
ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mwanza
pamoja na wadau wengine wa sekta ya maji.
Kwa
mawasiliano;
Mratibu
wa Tawi Mwanza
Simu:
+255 747 900 905 & +255 736 900 907
Barua
pepe: mwanzabranch@waterinstitute.ac.tz
Tovuti: www.waterinstitute.ac.tz
Mratibu
wa Tawi Singida
Simu:
+255 755 900 905 & +255 739 900 907
Barua
pepe: singidabranch@waterinstitute.ac.tz
Tovuti: www.waterinstitute.ac.tz
Posted on 28th April, 2020