News

TANGAZO LA MAHAFALI YA (45) 2021

Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wahitimu, wanafunzi, watumishi, wadau na watu wote kuwa Mahafali ya 45 ya Chuo
cha Maji yanatarajiwa kufanyika tarehe
26/11/2021 katika ukumbi wa Mlimani City. Kufuatia tangazo hili, wahitimu wote mnatakiwa kuhakiki majinayenu ambayo yanapatikana kwenye tovuti ya Chuo na kutuma marekebisho kwenye barua pepe registrar@waterinstitute.ac.tz

Aidha, wahitimu mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu kupitia account zenu za SIMS na kufanya malipo ya Tshs 32,000/=.
Fedha za tahadhari ambazo ni Tshs. 30,000/= zitatumika kulipia joho la mahafali hivyo utatakiwa kuongeza malipo ya Tshs 2000/= tu ili uweze kukamilisha uthibitisho wako. Mwisho wa kufanya uthibitisho ni tarehe 14/11/2021.
Nawatakia maandalizi mema.
Imetolewa na:
Ghanima Chanzi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

tangazo la mahafali

Posted on 08th October, 2021