UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF WATER
WATER INSTITUTE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF WATER
WATER INSTITUTE
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dkt. Batilda Burian, leo alitembelea
banda la Chuo cha Maji katika Maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi, na
Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga katika Viwanja vya shule ya Sekondari
ya Popatlal kuanzia tarehe 25 Mei na yataendelea mpaka tarehe 31 Mei
2024.
Wakati wa ziara yake, Dkt. Burian alipata maelezo kuhusu
huduma mbalimbali zinazopatikana Chuoni hapo ikiwemo programu za
mafunzo, huduma za utafiti na ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Chuo
cha Maji.
Kadhalika Mkuu wa Mkoa amevutiwa na elimu ya
teknolojia ya uvunaji sahihi wa maji ya mvua ambayo inafundishwa katika
banda la Chuo katika maonesho haya na amewataka Chuo cha Maji kuongeza
wigo zaidi wa kuongeza mashirikiano na vyuo vya nje ya nchi ambavyo
vinateknolojia za juu zaidi katika masuala ya maji.
Tunaendelea
kuwakaribisha wakazi wote wa jiji la Tanga kutembelea banda letu ili
kupata taarifa zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na chuo.