News

Chuo cha Maji Kuanzisha Programu Mpya kwa Ngazi ya Astashahada na Shahada

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt Adam O. Karia anawatangazia umma kuwa, Chuo kimeongeza kozi mpya za mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za Shahada (Degree) na Stashahada (Diploma) katika fani mbalimbali.

Lengo la kuanzishwa kwa kozi hizo mpya kunalenga kukidhi mahitaji ya jamii kwa sasa na baadae, pia kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya maji kupitia uzalishaji wa wataalam mahiri na wenye weledi sahihi.

Fani hizi mpya zilizoanzishwa zimeshapata ithibati kutoka Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE) na zitaanza kutolewa kuanzia mwaka wa masomo 2022/2023 yaani muhula utakaonza Oktoba, 2022. Kozi hizo ni kama ifuatavyo;

1. Bachelor Degree in Community Development for Water Supply and Sanitation

2. Bachelor Degree in Hydrogeology and Drilling

3. Bachelor Degree in Engineering Hydrology

4. Bachelor Degree in Sanitation Engineering

5. Ordinary Diploma in Sanitation Engineering

Posted on 04th February, 2022