News

Ujenzi wa kutanua majengo ya Chuo cha Maji kuanza hivi karibuni

Hatua hiyo inaashiriwa na ujio wa kampuni ya watalaam kutoka Mhandisi Consultancy na kampuni washauri walizoambatana nazo zaidi ya mbili, katika kuhakikisha kazi ya usanifu wa miundombinu iliyopo inafanyika ili kufanya ushauri elekezi kwa mkandarasi atakaetekeleza ujenzi huu.
Hii ni hatua muhimu sana kwa kukiongezea uwezo Chuo cha Maji na kuhakikisha adhma ya Serikali kupitia Wizara ya Maji inatimia katika kukiinua Chuo hiki kinachotoa wataalamu muhimu sana wanaotumikia Sekta ya Maji Nchini.
Asante sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli

Posted on 09th February, 2021