News

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Chuo cha Maji na Kongamano la Tatu la Kisayansi la Kimataifa la Maji yafana.

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Chuo cha Maji na Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kisayansi la Maji yanafanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 31 Januari hadi tarehe 2 Februari 2024.

Maadhimisho haya yalifunguliwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Katika hotuba yake, Rais Kikwete alipongeza jitihada zinazofanywa na Chuo cha Maji katika kukuza sekta ya maji nchini. "Katika miaka 50 ya chuo cha maji ni ni ishara ya kuimarika kwa kutengeneza watumishi mahiri wanaohudumu katika shughuli mbalimbali za kisekta," ameeleza Rais Kikwete.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Maji, Dkt. Adam O. Karia, ameeleza kuwa Chuo cha maji kinajivunia kuzalisha zaidi ya wataalamu 6,000 wenye ubora mkubwa na wanaoleta tija katika sekta ya maji. "Chuo cha Maji kinaahidi kuendelea kutengeneza wataalamu wengi zaidi ili kukidhi mahitaji ya sekta ya maji nchini," amesema Dkt. Karia.

Maadhimisho hayo yanahudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi. Kongamano hili lilitoa fursa kwa washiriki kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Maji, ikiwemo changamoto na fursa zinazoikabili sekta hiyo.

Posted on 01st February, 2024