News

Mkuu wa Chuo cha Maji amesaini na kukabidhiwa hati ya umiliki wa eneo la Chuo cha Maji Kampasi ya Singida

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia (aliyeshika nyaraka) mapema leo tarehe 25/03/2024 amesaini na kukabidhiwa hati ya umiliki wa eneo la Chuo cha Maji Kampasi ya Singida lenye ukubwa wa Ekari 41.5. Eneo hili lipo katika Manispaa ya Singida eneo la Mwankoko. Mkuu wa Chuo ameambatana na Mwanasheria wa Taasisi Wakili Adeline Roghat( wa mwisho kushoto). Eng. Stephen Alphayo ambaye ni Meneja wa Kampasi ya Singida na wa pili kulia ni Msajili wa Hati (M) Singida Bw. Sylvian Musiba. Kupatikana kwa eneo hili ni juhudi za makusudi kabisa za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Wizara yetu mama ya Maji inayosimamiwa na kiongozi wetu mahiri Mhe. Jumaa Hamidu Aweso Waziri wa Maji na viongozi wote waandamizi wa sekta kwa ujumla. Tunashukuru na kuthamini mchango huu katika taasisi ya elimu kwani bila kumilikishwa ardhi hatuweza kujipanua katika kuendeleza kutoa huduma bora kwa watanzania.

Posted on 25th March, 2024