News

Uzinduzi wa Kongamano la Kisayansi la Maji 2022

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wataalamu na wadau wa sekta ya maji kwa ujumla kushirikishana ujuzi na taaluma kuweza kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya maji kwa pamoja. Amesema Serikali kupitia Wizara ya Maji itahakikisha inawapa msaada wa hali na mali ili kuwezesha malengo maalumu ambayo ni pamoja na kumtua mama ndoo ya maji inafikiwa.

Mheshimiwa Naibu Waziri ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la kisayansi la maji lililofanyika jijini Dar es salaam leo Aprili 4, 2022. Aidha, Amekipongeza Chuo cha Maji kwa kuandaa kongamano hilo na kuwa msaada mkubwa katika kuwaandaa wataalamu wanaohudumu katika sekta ya maji nchini.

Posted on 04th April, 2022