News

Chuo cha Maji wamekutana na Wataalam wa Kituo cha Utafiti wa kuondoa madini ya Flouride kwenye maji kilichopo Ngurdoto

Chuo cha Maji tarehe 27/01/2020 wamekutana na Wataalam wa Kituo cha Utafiti wa kuondoa madini ya Flouride kwenye maji kilichopo Ngurdoto jijini Arusha.

Ziara hii ni katika kutekeleza agizo la Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso (Mb), kuwa Chuo sasa kitumike kikamilifu kufanya tafiti za kutatua matatizo ya Sekta ya Maji Nchini.

Aidha pande zote mbili zimekubaliana kwa pamoja kuanza maramoja tafiti mbalimbali za kutafuta suluhu ya kuondoa kiasi kikubwa cha madini ya Flouride, Arsenic, Iron na Manganese ambayo ni changamoto kubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Posted on 29th January, 2021