News

HISTORIA MPYA YAANDIKWA LEO TAREHE 12/11/2021 MJINI UNGUJA ZANZIBAR.

Mapema leo Chuo cha Maji na Mamlaka ya Maji Zanzibar wameingia katika historia kubwa ya kukubaliana na kusaini Mkataba wa Makubaliano ( Memorandum of Understanding) katika kuanzisha na kuendeleza mashirikiano katika masuala ya Mafunzo, Utafiti, Ushauri wa Kitaalam na Ubunifu. Lengo ni kuhakikisha Mamlaka ya Maji Zanzibar inanufaika na uwepo wa Chuo cha Maji lakini pia Chuo kinafaidika na fursa zilizopo katika Mamlaka hiyo na kuhakikisha ile Zanzibar ya Blue inafikiwa kwa mafanikio ya haraka yatakayosaidia Taasisi hizi kufanya mabadiliko chanja kwa haraka zaidi.
Mkuu wa Chuo Dkt Adam O. Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dkt. Salha Kassim wamesaini mkataba huo tayari kuanza kushirikiana mara moja.

Posted on 12th November, 2021