News

​Mkuu wa Mkoa wa Tanga atembelea banda la Chuo cha Maji

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dkt. Batilda Burian, leo alitembelea banda la Chuo cha Maji katika Maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi, na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga katika Viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal kuanzia tarehe 25 Mei na yataendelea mpaka tarehe 31 Mei 2024.

Wakati wa ziara yake, Dkt. Burian alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana Chuoni hapo ikiwemo programu za mafunzo, huduma za utafiti na ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Chuo cha Maji.

Kadhalika Mkuu wa Mkoa amevutiwa na elimu ya teknolojia ya uvunaji sahihi wa maji ya mvua ambayo inafundishwa katika banda la Chuo katika maonesho haya na amewataka Chuo cha Maji kuongeza wigo zaidi wa kuongeza mashirikiano na vyuo vya nje ya nchi ambavyo vinateknolojia za juu zaidi katika masuala ya maji.

Tunaendelea kuwakaribisha wakazi wote wa jiji la Tanga kutembelea banda letu ili kupata taarifa zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na chuo.

Posted on 30th May, 2024