News

TAARIFA YA MAHAFALI YA (47) YA MWAKA 2023

Mkuu wa Chuo cha Maji anawatangazia wahitimu, wanafunzi, watumishi, wadau na watu wote kuwa Mahafali ya 47 ya Chuo cha Maji yanatarajiwa kufanyika tarehe 02/11/2023 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kufuatia tangazo hili, wahitimu wote mnatakiwa kuhakiki Majina yenu kwenye mfumo wa SIMS yasomeke kama yalivyo katika cheti cha kumaliza kidato cha nne kuanzia leo tarehe 13/09/2023 hadi 30/09/2023. Pia hakikisha taarifa zote muhimu zimejazwa kwa usahihi ikiwemo mwaka wa kuzaliwa, sanduku la posta, mwaka wa kuanza masomo na picha ya passport size yenye kivuli cha bluu. Marekebisho yote ya majina yatumwe kwenye barua pepe: dass@waterinstitute.ac.tz.

Aidha, wahitimu mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu kupitia account zenu za SIMS kwa kulipia kiasi cha Tsh. 42,000/= kwa ajili ya Joho la mahafali ili kuweza kukamilisha uthibitisho wenu. Mwisho wa kuthibitisha ni tarehe 21/10/2023.

Posted on 15th September, 2023