News

​Chuo cha Maji wakishirikiana na Chuo cha Shinshu cha nchini Japan watoa msaada wa mtambo wa kuchuja na kuondoa floride

Chuo cha Maji wakishirikiana na Chuo cha Shinshu cha nchini Japan, na Chuo kikuu cha Dar es Salaam wametoa msaada wa mtambo wa kuchuja na kuondoa floride kwenye maji kwa wakazi wa kijiji cha Lemanda, Kata ya Oldonyosambu, Wiliya ya Arumeru Mkoani Arusha. Msaada huo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Shinshu na kuleta matokeo chanya, ambapo utafiti huo bado unaendelea. Hafla ya makabidhiano ya mtambo huo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa Japan nchini Mheshimiwa Yashushi Misawa, Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam O. Karia, na Viongozi wa Serikali wilayani Arumeru.

Posted on 27th January, 2023