News

RAIS MWINYI AWAPONGEZA CHUO CHA MAJI

Mapema leo tarehe 14/09/2022 Mjini Unguja katika ufunguzi wa Kongamano la Maji Zanzibar linalofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chuo cha Maji na kumtaka Mkuu wa Chuo hiko Dkt. Adam O. Karia kuendelea kutoa huduma zake Zanzibar kama ambavyo kimeanza katika kuisaidia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kufunga mfumo wa kisasa wa kuendesha shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo unaojulikana kama ILMS yaani Integrated Leakage Management System.

Dkt. Adam O. Karia alielezea mfumo wa ILMS na namna ambavyo umeleta ufanisi kwenye mamlaka ya Maji Zanzibar.

Posted on 14th September, 2022