TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO MUHULA WA MWEZI MACHI

Mkuu wa Chuo cha Maji anawakaribisha wahitimu wote wa kidato cha Nne kuanzia mwaka 2021 kurudi nyuma, kutuma maombi ya kujiunga na Chuo cha
Maji kwa muhula
mpya wa masomo utakaonza mwezi Machi, 2023 katika ngazi
za Astashahada na Stashahada (yaani Basic Technician Certificate na Ordinary Diploma)
katika fani za;
1. Water supply and sanitation engineering na
2. Water quality laboratory technology
Sifa za kujiunga
Mwanafunzi awe amemaliza Kidato cha Nne, awe na ufaulu kuanzia alama D Nne na kuendelea, alama D Tatu ziwe kati ya masomo ya Sayansi yaani Hisabati, Fizikia, Kemia, Biolojia, Jiographia, Kilimo na Engineering Science.
aidha, D Mbili na National Vocational Award (NVA) level 3 katika eneo la Uhandisi na Rasilimali za Maji.
tuma maombi ya kujiunga na chuo bure, kwa njia ya mtandao kupitia www. waterinstitute.ac.tz
mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 8 machi 2023
kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba;
0673679352, 0747900904 na 0735900907
Posted on 20th February, 2023