News

Waziri wa Elimu afurahishwa na Ubunifu katika Chuo cha Maji

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amekipongeza Chuo cha Maji baada ya kupokea maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Maji na kujionea Mfumo uliobuniwa na Mwanafunzi wa Chuo hiko ukileta mafanikio makubwa katika kusaidia Mamlaka za Maji nchini kuendesha shughuli zake kidigitali ikiwemo kudhibiti mivujo, kudhibiti ujazo wa maji kwenye matenki, kudhibiti ubora wa maji, kudhibiti wateja na miundombinu nk.
Ametoa salamu hizo za pongezi alipotembelea banda la Chuo kwenye sherehe za kufunga maonesho ya NACTVET yanayotamatishwa leo kwenye Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Posted on 14th June, 2022